TAARIFA YA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA MSIMU WA MASIKA
MACHI-MEI 2024
Kipindi cha mvua ya Machi-Mei ni kipindi cha mvua za masika katika sehemu nyingi nchini.
Kiwango cha juu cha mvua (zaidi ya mm 300) hunakiliwa maeneo ya Ziwa Viktoria, Nyanda
za juu za Magharibi, Katikati na Kusini mwa Bonde la Ufa. Vilevile Mashariki mwa Bonde la
Ufa (pamoja na Nairobi) na mwambao wa Pwani.
Mvua nyingi inayozidi ile ya kawaida inatarajiwa maeneo ya Ziwa Viktoria, Nyanda za juu za
Magharibi, katikati, kaskazini na kusini mwa Bonde la Ufa. Pia maeneo ya nyanda za Mashariki
mwa Bonde la Ufa pamoja na maeneo ya Nairobi, Kaskazini Mashariki, Kusini Mashariki na
Kaskazini Magharibi. Kwa ujumla, viwango vya mvua karibu ya wastani (average) na ya
mwelekeo zaidi ya kawaida inatarajiwa kwenye maeneo ya Pwani na nyanda za chini za Kusini
Mashariki. Dhoruba za mara kwa mara zaweza tokea wakati wa msimu.
Katika msimu huu, kuna uwezekano wa maeneo mengi kupata mgawo wa mvua wenye ujumla
wa kuridhisha, isipokuwa kaskazini mashariki na kaskazini magharibi ambapo mgawo
unatarajiwa kukaribia ule wa kiwango cha kuridhisha. Msimu unatarajiwa kuanza mapema
ingawa kutakuwa na vipindi kavu mara kwa mara. Dhoruba za mara kwa mara zinawezatokea
katika baadhi ya sehemu za nchi. Kilele cha mvua kinatarajiwa mwezi wa Aprili katika sehemu
nyingi nchini isipokuwa sehemu za mwambao wa Pwani ambapo kilele kinatarajiwa kuwa
mwezi wa Mei.
Hali ya joto nchini inatarajiwa kuwa zaidi ya wastani (average) katika maeneo yote ya nchi na
yenye uwezekano mkubwa zaidi katika sehemu za pwani na Kaskazini mwa nchi.