Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Masika kipindi cha Machi – Mei, 2025
- Tathmini ya hali ya hewa msimu huu wa mvua za masika inaonyesha kwamba, viwango vya mvua ambavyo vinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi vinakadiliwa kuwa vya chini, hasa katika kanda za Mashariki ya Kenya na kaskazini ya mwambao wa Pwani. Hata hivyo, baadhi ya maeneo ya Magharibi mwa nchi na nyanda za chini za mashariki ya Kenya yanatarajiwa kuwa na mvua ya kiwango cha zaidi ya kawaida. Vilevile, kanda za juu ya kaskazini na katikati mwa bonde la ufa, nyanda za mashariki mwa bonde la ufa, Kusini na katikati ya pwani, kiwango cha mvua kinatarajiwa kuwa cha kawaida mpaka chini ya kawaida. Mgao wa mvua hizi unaonyesha kwamba, sehemu nyingi kwenye kanda za mashariki mwa nchi zinatarajiwa kuwa kavu kwenye mwezi wa Machi. Mgao huu unatarajiwa kuwa kileleni katika maeneo mengi nchini kwenye mwezi wa Aprili ila maeneo ya pwani kilele chake kinatarajiwa Mei, japo kiwango chake kitakuwa cha chini. Zaidi ya hayo, maeneo mengine nchini yana uwezekano mkubwa wa kupata mvua za dhoruba za mara kwa mara. Hali hii itakuwa imechochewa na hali ya joto (SSTS) kwenye bahari ya hindi, pasifiki na atlantiki na pia ushawishi wa mambo ya kijografia, na viashiria muonekano vinavyoathiri mwelekeo wa hali ya hewa nchini.
-
Mtazamo wa hali ya joto MAM 2025
- Kwa upande mwingine, utabiri wa joto unaonyesha kwamba eneo kubwa nchini msimu
huu, linatarajiwa kuwa na hali ya joto ya juu kuzidi wastani lakini viwango vyake
vinatofautiana kwa maeneo tofauti nchini. Kwa kuangazia maeneo ya kaskazini ya
nchi na baadhi ya sehemu za kusini zinatarajia hali ya joto kufikia nyusi za juu zaidi
ya maeneo mengine nchini.