MUKHTASARI

  • Kipindi cha mvua ya Machi-Mei ni kipindi cha mvua za masika katika sehemu nyingi nchini.Kiwango cha juu cha mvua (zaidi ya mm 300) hunakiliwa maeneo ya Ziwa Viktoria, Nyanda za juu za Magharibi, Katikati na Kusini mwa Bonde la Ufa. Vilevile Mashariki mwa Bonde la Ufa (pamoja na Nairobi) na mwambao wa Pwani.
  • Mvua nyingi inayozidi ile ya kawaida inatarajiwa maeneo ya Ziwa Viktoria, Nyanda za juu za Magharibi, katikati, kaskazini na kusini mwa Bonde la Ufa. Pia maeneo ya nyanda za Mashariki mwa Bonde la Ufa pamoja na maeneo ya Nairobi, Kaskazini Mashariki, Kusini Mashariki na Kaskazini Magharibi. Kwa ujumla, viwango vya mvua karibu ya wastani (average) na ya mwelekeo zaidi ya kawaida inatarajiwa kwenye maeneo ya Pwani na nyanda za chini za Kusini Mashariki. Dhoruba za mara kwa mara zaweza tokea wakati wa msimu.
  • Katika msimu huu, kuna uwezekano wa maeneo mengi kupata mgawo wa mvua wenye ujumla wa kuridhisha, isipokuwa kaskazini mashariki na kaskazini magharibi ambapo mgawo unatarajiwa kukaribia ule wa kiwango cha kuridhisha. Msimu unatarajiwa kuanza mapema ingawa kutakuwa na vipindi kavu mara kwa mara. Dhoruba za mara kwa mara zinawezatokea katika baadhi ya sehemu za nchi. Kilele cha mvua kinatarajiwa mwezi wa Aprili katika sehemu nyingi nchini isipokuwa sehemu za mwambao wa Pwani ambapo kilele kinatarajiwa kuwa mwezi wa Mei.
  • Hali ya joto nchini inatarajiwa kuwa zaidi ya wastani (average) katika maeneo yote ya nchi na yenye uwezekano mkubwa zaidi katika sehemu za pwani na Kaskazini mwa nchi.